Kufuatia mgogoro na vita vya maneno vinavyoendelea ndani ya chama tawala CCM,juu ya kada wa chama hicho Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuanza kampeni za chini chini za kugombea urais mwaka 2015,wadau na wasomi wamesikitishwa na mgogoro huo na kumuomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndio mwenyekiti wa CCM kuingilia kati ili kusafisha hali hiyo mbaya ya hewa.
Prof.Baregu ametoa maoni yake na kusema kama Mwenyekiti wa chama hicho hakuitisha mkutano wa dharura kulimaliza hili basi kutakuwa na mgawanyiko mkubwa wa chama hapo 2015 na CCM itaanguka vibaya.
Hivi karibuni kumekuwa na maneno mengi kwa viongozi mbali mbali wa CCM kumpinga Edward Lowassa na kampeni zake za chini chini kuwania nafasi ya urais hapo 2015 na kuna upande mwingine ukimsapoti kwa kiasi kikubwa na kudai Lowassa yupo sawa kabisa. Hivyo hali hii ndio inawasukuma wadau wa mambo ya kisiasa,wanachama na wasomi mbalimbali kumuomba Mwenyekiti kuliweka sawa suala hili kwa hofu ya chama kuharibikiwa huko mbele ambako kwa sasa imebaki miaka miwili tu kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi wa rais na wabunge.
0 comments:
Post a Comment