Viazi vitamu vikiwa vimejazwa kwenye ndoo na wafanyabiashara wakisubiri kuviuza maeneo ya Majengo Mjini Dodoma kati ya Barabara iendayo Manyoni Singida na ile ya Babati-Arusha.Vipimo vya ndoo badala ya mizani vimekua na upungufu mkubwa kwani humpunja mkulima na mnunuzi huku mfanyabiashara akizidi kuneemeka na vipimo hivyo.Tunaomba mamlaka husika kupitisha sheria ya kutumia mzani sasa badala ya kutumia ndoo.
Mteja wa viazi vitamu akijaribu kuulizia bei ya viazi hivyo ili apate kuvinunua kwa ajiri ya chakula nyumbani kwake.
Mfanyabiashara wa viazi vitamu akijaribu kuelewana bei na mteja wake.
0 comments:
Post a Comment