Wednesday, October 2, 2013

KWA HALI HII VITA DHIDI YA MALARIA ITAKUWA NGUMU

    Hii ni bustani ya mboga maeneo ya bonde la mto  Matarawe Mjini Songea Mkoa wa Ruvuma.Bustani hizi zipo nyingi sana katika mji huu wa Songea.Chakushangaza hapa ili kufanya uzio wa bustani hizi, ili mboga isiliwe na mbuzi au kuku wananchi hawa wameamua kutumia vyandarua vilivyogaiwa na Serikali bure ili wajikinge na mbu wa malaria na kutengenezea uzio huo kama ilivyokutwa na mpiga picha wetu huko mjini Songea.
     Kwa hali hii vita dhidi ya malaria itakuwa ngumu kwa kuwa wananchi hawaoni umuhimu wa kutumia vyandarua hivi na viongozi wa Serikali za mitaa hawajui wajibu wao kwa Serikali maana wanaangalia tu haya yakitendeka kwenye mitaa yao bila ya kuchukua hatua.Wananchi hawa wote wanastaili kufikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya mali za Serikali.
    Kwa kuwa wanaitia hasara kubwa  Serikali, maana inatumia fedha nyingi kutengeneza hivyo vyandarua na inatumia fedha nyingi kununua madawa ya malaria kutibu wananchi wake.
  Tunaomba mamlaka husika kufuatilia hili na kuwachukulia wananchi hawa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine kurudia vitendo hivi.

0 comments:

Post a Comment