"Dustbin" la takataka likiwa limejaa mpaka taka nyingine zikimwagika maeneo ya barabara ya Ali Hassani Mwinyi jirani na Ubalozi wa Kenya kwenye makutano ya Barabara ya Kaunda kuelekea Masaki.Kitendo cha mamlaka husika kuziacha takataka hizi kujaa na kumwagika kunatuvunja moyo sisi wananchi tulioitikia wito wa kutupa takataka katika vifaa hivi maalumu ili kuliweka Jiji letu la Dsm katika hali ya usafi.
Tunaomba Halmashauri za jiji la Dar es Salaam kuangalia upya utaratibu mzima wa kuzoa taka hizi kila zinapojaa na wasiziache mpaka zikamwagika hivyo hata nikitaka kutupa taka nyingine unashindwa uziweke wapi!
0 comments:
Post a Comment