Saturday, November 9, 2013

MAMA MZAZI WA DIAMOND: NAMKUBALI SANA PENNY KULIKO WEMA SEPETU.


    Kufuatia tetesi za msanii maarufu wa Bongo Fleva nchini Nassibu Abdul "Diamond" kurudiana na msanii maarufu wa Bongo Movie Wema Sepetu mama mzazi wa Diamond,Sanura Kassim "Sandra" amefunguka mwishoni mwa wiki akiwa nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar es Salaam kuwa yeye hafahamu chochote juu ya Wema Sepetu kurudiana na mwanae Diamond. Ila anapata habari hizo kupitia magazeti na kuangalia picha mbalimbali katika mitandao zikielezea kurudiana kwa Diamond na Wema Sepetu.
   Akiendelea kufunguka mama huyo wa msanii anayetamba na ngoma yake mpya kwa sasa ya "Number One"amesema hamtaki kabisa staa wa Bongo Movie Wema Sepetu arudiane na mwanae kwa kuwa anamkubali kwa sana Penniel Mungilwa "Penny".
    Hata hivyo mama mzazi huyo wa Diamond ametabainisha kuwa bado hajakaa na mwanae na kuzungumzia kuhusu suala hilo hivyo akipata wasaa na kuzungumza naye atatoa tamko lake.

0 comments:

Post a Comment