Mgogoro uliozuka ndani ya chama chenye nguvu ya
upinzani hapa nchini CHADEMA, kati ya chama hicho na Naibu Katibu Mkuu wake
Zitto Kabwe (Mbunge) unaleta hofu kubwa juu ya hatma ya chama hicho hapa
nchini.
Mgogoro huo unatokana na walaka uliosambaa
mitandaoni usemao "Ripoti ya Siri juu ya Zitto Kabwe" katika ripoti
hiyo imeelezwa kuwa chama chake kilikuwa kinamchunguza Zitto kuanzia mwaka 2008
hada mwaka 2010 na kubaini kuwa Naibu Katibu Mkuu huyo alikuwa anapokea fedha
kutoka chama tawala CCM na kushirikiana na Usalama wa Taifa ili kuivuruga
CHADEMA. Katika ripoti hiyo mtu mwingine anayetajwa kufanya hujuma hiyo ni
Dr.Kitila Mkumbo mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA.
Kufuatia taarifa hizo Zitto amekanusha vikali
tuhuma hizo na kumwandikia barua Katibu Mkuu wa chama hicho Dr.Willbrod
Slaa ili azikanushe,aseme kama ujumbe huo ni wa CHADEMA au kikundi
cha watu wachache wenye lengo la kumchafua kisiasa na kama itagundulika
kuwa taarifa hiyo ni ya kikundi cha watu wachache wenye lengo la kumchafua
kisiasa Zitto amehaidi kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watu hao
walioandika ujumbe huo.
Kufuatia sakata hilo hofu kubwa inazidi kutanda
CHADEMA endapo Dr.Slaa atajibu na kusema ujumbe huo ni halali na umetolewa na
CHADEMA na unaukweli ndani yake na wakauthibitisha.Hapo sasa sijui Zitto
atachukua hatua gani na CHADEMA watachukua hatua gani acha tusubiri tuone
mwisho wa sakata hili.
0 comments:
Post a Comment