Askari wa usalama barabarani akikagua gari namba T 346 APS aina ya Benz lililopata ajali eneo la Kinondoni kwa Manyanya tarehe 23/03/2013 majira ya asubuhi baada ya kugongana na daladala la Buguruni/Msasani halipo pichani. Makosa yalikuwa ni kwa dereva wa gari dogo la Benz ambaye alikuwa akitokea Kinondoni Makaburini na kuingia barabara ya Kawawa bila kuangalia vema kama kuna gari hilo la daladala linakuja na yeye alitakiwa asimame mpaka lipite.Ajali hii isingetokea kama dereva wa gari dogo angechukua tahadhari mapema.Tunaendelea kuwasihi madereva kuchukua tahadhari na kuwa makini wanapokuwa barabarani hii itasaidia sana kupunguza ajali ambazo kama madereva wangechukua tahadhari zisingeweza kutokea.
0 comments:
Post a Comment