Mtangazaji maarufu Tanzania Julius Nyaisanga maarufu kama Uncle J au Babu wa Kimanzichana amefariki dunia siku ya Jumapili tarehe 20/10/2013 mjini Morogoro,amefariki akiwa kama mmoja wa wakuu wa idara wa Abood Televisheni inayomilikiwa na Abood Media ya Morogoro.
Hakika tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu sana katika fani hiyo ambaye bado alikuwa anahitajika katika kuwafundisha vijana wa sasa chipukizi katika kazi ya utangazaji.
Nachokiona kwa sasa ni hazina aliyotuachia mtangazaji huyu,hasa katika ubunifu wa vipindi mbalimbali redioni huku akibadilika kutokana na wakati unavyokwenda.Ubunifu wake ukianzia redio Tanzania sasa TBC na kuundeleza Radio One.
Hivyo tunaomba wataalamu mbalimbali kukaa na kutengeneza " documentary CD "ya vipindi vyake mbalimbali alivyokuwa anaviendesha na kivitia mbwembwe na kuvutia watu wengi kwa Radio Tanzania kuna Klabu Raha Leo Show,Misakato,Bendi Zetu,Top Ten Showna Disco Show na Radio One kuna kipindi cha Mambo Mseto na Hizi nazo na vipindi vingine vingi,vile vile ameweza kuanzisha misemo mingi sana katika Kiswahili kama "ngoma za kuruka majoka-Break dance",ngoma za kufokafoka muziki wa rap,,ngoma za kuruka misumari muziki wa reggae,nyuzi bin nyuzi pale gitaa linapopigwa vizuri kwenye wimbo. Hiyo yote ni hazima kwa vizazi vijavyo na inaweza kutumika katika kufundishia vijana wetu katika vyuo vyetu mbalimbali vya habari hapa nchini na hata nje ya nchi yetu.
Kwa maana hiyo Watanzania tusidharau kabisa kazi za mtangazaji huyu kwani ni hazina kubwa kabisa katika Taifa letu.
0 comments:
Post a Comment