Vigogo sita wa CCM wanaowania nafasi ya Urais mwaka 2015 wameitwa na kuhojiwa katika kamati Ndogo ya Maadili ya CCM kwa shutuma za kukiuka maadili.Vigogo hao ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu) Steven Wasira, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye,Waziri wa Manbo ya Nchi za Nje Bernard Membe,Waziri wa zamani wa Nishati na Madini Willium Ngereja na Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia January Makamba.Taarifa za ndani toka chama hicho zinadai barua za kuwaita vigogo hao tayari zimeshaanza kusambazwa kwenda kwa vigogo hao na kikao hicho kitakaa mjini Dodoma tarehe 14 Feb,2014.
0 comments:
Post a Comment