Friday, January 31, 2014

URAIS 2015:MALECELA AMCHANA LIVE LOWASSA.




Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Ndugu John Samweli Malecela amefunguka na kukemea waziwazi kitendo cha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kuanza kampeni za kuwania Urais 2015 mapema kabla ya muda wake kupangwa. Akihojiwa nyumbani kwake mjini Dodoma jana Malecela alisema kitendo hiko kinakigawa Chama na kinapaswa kukemewa na Sekretarieti ya chama hicho bila kumwogopa mtu.
Malecela alienda mbali kwa kumsifu Paul Makonda Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana CCM(UVCCM) kwa kumkemea Lowassa kuwa anakiyumbusha chama kwa kufanya kampeni za Urais 2015 kabla ya muda. Alihoji wakubwa wapo wapi hata wakamuachia kijana anahangaika peke yake kukemea hili.
Alisema amepata fulana mbili zilizoandikwa "Friends of Lowassa" na kudai fulana hizo zimesambazwa nchi nzima. Akahoji inamaana utakapofika wakati wa kugombea huyu atakuwa amejiimarisha vya kutosha na atakuwa ametumia fedha nyingi kujipigia kampeni mapema na hivyo kuwashinda wenzake kwa urahisi.Hii sio sawa kabisa akemewe kwa vitendo hivyo alihitimisha mkongwe huyo wa siasa hapa nchini.

0 comments:

Post a Comment