Dr.Juma Ngasongwa Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara amenusurika katika ajali ya gari iliyotokea juzi jioni maeneo ya Picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani.Ajali hiyo ilitokea baada ya kugongana na lori la Tanesco aina ya Mitsubishi lililokuwa likiendeshwa na Hussein Mnemwa.Dr.Ngasongwa alikuwa akitokea Dodoma kuja Dar es Salaam na gari aina ya Toyota Rav 4 aliyokuwa akiendesha yeye mwenyewe.
Baada ya ajali Dr.Ngasongwa alipelekwa Hospitali Teule ya Tumbi Kibaha na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment