Wanasayansi wa Uswisi wametoa
ripoti ya uchunguzi wao jana kuhusiana na kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Palestine Liberation
Organisation (PLO) Yasser Arafat kilichotokea tarehe 11 Novemba,2004.
Wachunguzi hao wamesema mabaki ya
mwili wa Yasser Arafat yamekutwa na kiwango kikubwa cha mionzi ya polonium
ambayo ni sumu na inaathari kubwa kwa mwili wa mwanadamu.Lakini hawajaweka bayana kuwa sumu hiyo ndio sababu iliyopelekea umauti kwa kiongozi huyo.
Kutokana na
taarifa hiyo kunaonesha kuwa kifo cha mwanaharakati huyo huenda kilipangwa kwa
makusudi na majasusi ili kumuangamiza ingawa bado kuna utata ni wakati gani njama hizo zilifanyika kwa bwana Arafat.
Taarifa za awali za kifo chake
kabla ya uchunguzi huo kufanyika zilisema,Yasser
Arafat alikufa kwa ugonjwa wa shinikizo la damu huku Wapalestina nao
wakidai kuwa Waisrael wamemuua Arafat kwa kumuwekea sumu.
Kwa sasa bado nchi
mbalimbali duniani hazijatoa matamko yao
kuhusiana na ripoti hiyo ya uchunguzi toka kwa Wanasayansi hao wa Uswisi.
0 comments:
Post a Comment