Timu ya Azam ya Chamazi Jijini Dar es Salaam na
timu ya Mbeya City ya Mbeya jana zimemenyana
vikali katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika uwanja wa
Chamazi Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kutoka sare ya
mabao 3-3
Kwa ushindi huo timu zote mbili
zimefikisha pointi 27 hivyo Azam imekuwa ya pili katika ligi ikiipiku Mbeya City
kwa wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa hivyo Mbeya City
kushika nafasi ya tatu na Yanga FC kuongoza ligi kwa kuwa imefikisha pointi 28
baada ya kuifunga JKT Oljoro 3-0.
Mabao ya Azam yamefungwa na Humphrey
Mieno dakika ya 13,John Bocco(Adebayor) dakika ya 60 na Kahmis
Mcha(VIalli) dakika ya 83 na mabao ya Mbeya City yote matatu yamefungwa na
Mwagane Yeya(Morgan) dakika ya 30,52 na 73.
Baada ya Mbeya
City kufunga bao la tatu dakika ya 73
na kuongoza kwa mabao 3-2 kuliwafanya Azam wachanganyikiwe na
kujihisi wanalala katika uwanja wao wa nyumbani hivyo walipigana kufa na kupona
na kusawazisha bao bao hilo
dakika ya 83 zikiwa zimebaki dakika 7 tu kabla ya mpira kwisha.
0 comments:
Post a Comment