Wema Sepetu akielekea makaburini peke yake bila hata mpambe mmoja wa
Bongo Movie kuwa pembeni yake kumsindikiza wakati wa mazishi huko Zanzibar.
Hatimaye
Wema Sepetu ambaye alikuwa Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie
kwa sasa amefunguka na kuzungumzia hatua ya wasanii wenzake wa Bongo Movie
kumsusia msiba wa baba yake mzazi Balozi Issac Abrahamu Sepetu
siku chache zilizopita.Amesema amesikitishwa sana kwa kitendo hicho na kusema
kimesababisha alie mara mbili kwanza kwa kufiwa na baba yake na pili kwa
kutoonekana kwa wasanii wenzake msibani.
Wema kwa hali ya
masikitiko amewaambia wasanii wenzanke kuwa wangekuja kwanza wakamfariji kwa
kumzika baba yake na kasha kwa yale makosa yake aliyofanya wangemuita na
kumuambia ili ajirekebishe.Hata hivyo amejifariji kwa kusema kuwa pamoja na
kutokuja kwao hawajampunguzika kitu.
Nao wasanii wa
Bongo Movie wakizungumzia hali hiyo wamesema hilo ni kama fundisho kwa
mlimbwende huyo.Wamedai amekuwa na tabia mbaya ya kutohudhuria katika misiba ya
wasanii wenzake wakitoa mfano kuwa Wema hakuhudhuria msiba wa marehemu
Sajuki,msanii Dude naye alilalamika kutokumuona Wema alipofiwa na mama yake
mzazi na hata hakuja kutoa pole.Mbali na Dude naye Steve Nyerere alimlalamikia
msanii huyo kwa kutoonekana katika msiba wa mtoto wake.
Wasanii pekee
wa Bongo Movie waliojitokeza kwenye msiba huo ni Yobnesh Yusuph
"Batuli",Elizabeth Michael "Lulu", Kajala Masanja,Mahsein
Awadhi"Dokta Cheni,Salumu Mchoma "Chiki" na Jaqueline Wolper.
0 comments:
Post a Comment