Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya
CHADEMA Halima Mdee amewaka jana ndani ya Bunge kuhusu sintofahamu
inayojitokeza kwa Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi kuhusiana na alama za
ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambao wapo kwenye mitihani yao katika
kipindi hiki.Hali hiyo ya sintofahamu inakuja kutokana na maelezo tofauti
yanayotolewa na Wizara hiyo kuhusiana na marekebisho ya alama za ufaulu kwa
wanafunzi wa kidato cha nne.
Taarifa za awali zilizotolewa na Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo zilieleza kuwa daraja la sifuri limefutwa kabisa kwa kidato
cha nne na kutakuwa na daraja la tano.
Lakini katika kipindi cha maswali na majibu
Bungeni juzi Mbunge Viti Maalum (CCM) Catherine Magige aliuliza kuhusiana
na kufutwa kwa daraja sifuli ni kama njia ya kuwaokoa wanafunzi wanaofeli
kidato cha nne.Naibu Waziri Philipo Mahugo alijibu kuwa Wizara
haijafuta daraja sifuli madaraja yaliyopo ni la kwanza,la pili,la tatu,la nne
na la sifuli.
Kutokana na kauli hiyo ya Naibu Waziri
juzi imepelekea Mbuge Halima Mdee kuomba ufafanuzi jana Bungeni kwa kudai
maelezo yanayotolewa Bungeni hapo yana tofauti kubwa na maelezo kutoka kwa
Katibu wa Wizara hiyo,hivyo kuna uongo katika taarifa hizi na kama Naibu Waziri
amelidanganya Bunge anaomba muongozo juu ya hatua
zitakazochuliwa kwake. Hali hiyo ilimfanya Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Willium Lukuvi aingilie kati na kutoa ufafanuzi kuwa anachozungumza
Waziri ndio kauli sahihi ya Serikali na siyo Katibu Mkuu wa Wizara lakini kama Serikali watalifanyia kazi na kuja na kauli ya
Serikali.
Naye Naibu Spika wa Bunge Ndijobu Ndugai aliiomba Serikali ilifanyie kazi jambo
hili na kuleta kauli ya Serikali haraka maana kidato cha nne wapo kwenye
mitihani yao kwa sasa hivyo wanahitaji kujua
hatma yao
katika mitihani hii wanayoifanya.
0 comments:
Post a Comment