Ester Bulaya Mbunge
Viti Maalum(CCM) ambaye alitoa maelezo binafsi Bungeni juzi kuhusiana na hali
ya dawa za kulevya nchini na sheria zake zinavyopwaya na kuwalinda wafanyabiashara wa dawa za kulevya amesema kuwa haogopi kufa. Katika taarifa yake hiyo
Bungeni Ester ametoa vielelezo mbalimbali vya jinsi wafanyabiashara hao
wanavyotamba kwa kuwa na uwezo wa kifedha na kufanya lolote ili wasitiwe
nguvuni na mkono wa sheria. Kwenye maelezo yake ametaja kesi mbalimbali za
wauza unga jinsi walivyokwepa hukumu kwa mahakama kupindisha sheria kwa
makusudi ili kuwaokoa.Vile vile amemtaja mwanadada Masogange
jinsi anavyoendelea kutanua uraiani hali alipitisha mabegi takribani kumi na
mbili ya viambata vya kutengenezea heroin katika Uwanja wa Ndege wa
Mwalimu Julius Nyerere Dar Es Salaam na kwenda kukamatwa nchini Afrika
Kusini na sheria za dawa za kulevya hazimgusi kwa lolote toka arudi hapa
nchini.Ester amesema sheria zina mapungufu na ameomba sheria za dawa za
kulevya ziangaliwe upya na kuwe na Mahakama maalumu ya dawa za kulevya.
Baada ya
maelezo yake hayo Bungeni juzi Ester Bulaya amesema amepokea simu
mbalimbali ikiwemo za kumpa pongezi kwa kulivalia njuga janga hili la dawa za
kulevya na simu nyingine za kumuasa aachane kabisa na kazi za wauza unga
vinginevya atapoteza maisha yake wakijaribu kufananisha hatua aliyochukua ni kama
ya marehemu Amina Chifupa ambaye alisema yupo tayari kuwataja wauza unga
Bungeni na baadaye alikumbwa na umauti kabla ya kuwataja wauza unga hao
Bungeni.Mbunge Ester Bulaya amesema haogopi kufa kwani anamtegemea sana Mungu
na kuongeza hata kama wakinipiga namna gani,wanipe sumu kali namna gani kama
Mungu hataki nife basi siwezi kufa hivypo sitishiki kwa lolote mimi nitakufa
kwa mpango wa MUNGU.
0 comments:
Post a Comment