Msanii Diamond wa kwanza kulia akiwa na mtangazaji wa Clouds TV wa
kipindi cha Take One Zamaradi Mtetema katikati na rafiki wao wa karibu.
Msanii Nasibu Abdul-Diamond ameweka wazi
kuwa yeye yupo tayari kwa lolote kwa hatua yake ya kurudiana na Miss Tanzania
2006 ambaye pia ni msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu. Hali hiyo imejitokeza
baada ya msanii huyo kuwa karibu na mlimbwende huyo kwa sasa ambaye walikuwa
wamemwagana katika mahusiano yao
ya kimapenzi.
Baada ya kuachana na
dada huyo inasadikiwa kuna mtu alikuwa karibu na binti huyo baada ya kuachana
na Diamond akimuwezesha kuishi hapa mjini.Hivyo basi alipoulizwa kuwa
analichukuliaje hilo pale ambapo sasa anajisogeza karibu na binti huyo hali
kuna mtu wake wa karibu ambaye anaweza kumfanyia kitu mbaya?Diamond alisema
kuwa yeye ni mtu anayejiamini haogopi na yupo tayari kwa lolote kwani
alishawahi kufungwa miezi miwili Gereza la Keko kwa kugombania demu wa mtu.
Kauli yake hiyo inaonesha wazi kuwa Diamond yupo
tayari kwa lolote kwa ajili ya penzi la Wema Sepetu na wala hatishiki na mtu yeyote.
0 comments:
Post a Comment