Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana alimtembelea na kumjulia hali Mjumbe wa
Tume ya Katiba Dkt Sengondo Mvungi aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kitengo cha mifupa MOI.Mjumbe huyo alikumbwa na mkasa
wa kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba Msakuzi nje kidogo ya jiji la Dar es
salaam na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi siku ya Jumamosi 2/11/2013
saa sita usiku na kumjerui vibaya kwa mapanga sehemu za kichwani na usoni.
Katika tukio hilo mbali na kumjerui Dkt.Mvungi watu hao walichukua
bastola yake fedha na laptop anayofanyia kazi.Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Tume
ya Katiba Jaji Warioba alisema wao kwa sasa wanasubiri ripoti kutoka kwa vyombo
vya dola.
Taarifa za awali toka vyombo vya
dola zinasema tukio hilo
ni la wizi tu halina uhusiano na kitu chochote kuhusiana na shughuli anazofanya
Dkt.Mvungi.
Dkt.Mvungi
akiingizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana Jumapili
akitokea Hospitali ya Tumbi Kibaha.
0 comments:
Post a Comment