Mwanaharakati wa kutetea haki za
wanyama nchini Mchungaji Clement Aloyce akiongea na waandishi wa habari
kuhusu umuhimu wa wananchi kutunza na kuwalinda wanyama pori hasa tembo ambao
kwa sasa ndio wanauwawa kwa kiasi kikubwa na wapo hatarini kutoweka.Mchungaji
Aloyce aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa
Habari Maelezo jana Jijini Dar es Salaam.Mchungaji huyo amesema kwa sasa vita
yake kubwa katika kuwalinda tembo hao ipo katika kufanya maombi kwa nguvu zote
ili Mungu aweze kusaidia kulinda wanyama pori hawa hasa tembo ili wasiweze
kuuwawa na majangili.Pembeni upande wa kushoto ni Afisa Wanyama Pori Mkuu toka
Wizara ya Maliasili na Utalii Bw.John Muya.
0 comments:
Post a Comment