Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Ndugu Abdulrahaman Kinana amesikitishwa na taarifa ya kifo Cha Mjumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba Dr Sengondo Mvungi kilichotokea Jana katika Hospitali
ya Millpark nchini Afrika ya Kusini.
Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu
Mkuu anawapa pole wanafamilia, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Warioba na Uongozi wa Chama Cha NCCR-Mageuzi. Hakika Taifa limepoteza Mtaalamu
wa Sheria, Kiongozi Mzalendo na hodari katika kipindi ambacho mawazo yake
yanahitajika kwa kiasi kikubwa kuliendeleza Taifa hili.
Mungu aiweke roho
ya marehemu mahali pema peponi.
0 comments:
Post a Comment