Kocha Mkuu wa timu ya Azam FC
Stewart Hall raia wa Uingereza jana ameachia wadhifa huo baada ya Uongozi wa
Azam kukataa kumuongezea mkataba mwingine baada ya kumalizika kwa mzunguko wa
kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacaom Tanzania Bara.
Kocha
Stewart ameiwezesha timu ya Azam kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa
imeshika nafasi ya pili.Nafasi ya kwanza ikishikwa na bingwa mtetezi Yanga FC
ya Dar es Salaam na huku nafasi ya tatu ikishikwa na Mbeya City
toka Mbeya.
Hata hivyo
Stewart wakati anaaga wachezaji wake jana na benchi la ufundi baada ya mchezo
wao na Mbeya City jana waliotoka sare ya mabao
3-3 amesema ameondoka Azam kwa roho safi
na baraka zote za Uongozi kwa kuwa amepata kazi sehemu nyingine.
Hata hivyo
taarifa za ndani toka Azam FC timu yenye mafanikio makubwa hapa Tanzania
zilinyetisha kuwa Stewart ilikuwa lazima aondoke,alikuwa anasubiriwa tu amalize
mzunguko wa kwanza maana angeondoka katikati ya mzunguko wa kwanza
ingekuwa ni tatizo kubwa kwa kuwa ingeweza kuwaathiri wachezaji
kisaikolojia.
Bado
haijajulikana kocha huyo ambaye alishawahi kutimuliwa mara ya kwanza katika
timu hiyo ya Azam siku za nyuma na kurejeshwa tena Desemba mwaka
jana ataelekea wapi baada ya kutoka hapo Chamazi Complex.
0 comments:
Post a Comment