Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athumani.
§ MNAMO
TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO
KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. KASSIM
SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MKAZI WA DSM ALIFARIKI DUNIA
WAKATI AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALIFAHAMIKA JINA KWA
MUJIBU WA HATI YAKE YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 KUTOKA DSM KUELEKEALILONGWE NCHINI MALAWI .
§ MAREHEMU
ALIKUWA ANASAFIRI AKIWA KATIKA BASI LA TAQWA LENYE
NAMBA ZA USAJIRIT.319 BLZ AINA YA NISSAN KWA MUJIBU WA
TIKETI YAKE ILIYOKUWA NA JINA LA KASSIM MUECK MICHAEL, AKIWA
NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS,T-SHIRT MOJA NYEUSI,RABA JOZI
MOJA RANGI NYEKUNDU,MKATE MMOJA ,MKOBA MDOGO WA KIUNONI,VACCINATION CARD MBILI
ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RANDI MBILI SARAFU ZA AFRIKA KUSINI NA
MIFUKO SITA YA RAMBO RANGI NYEUSI.
§ AWALI
BASI HILO BAADA YA KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA
ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU
ZA KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI
YA GARI HUKU HALI YAKE YA KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA.
§ WAHUSIKA
WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA
KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU.
HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA.
§ KUFUATIA
DALILI ALIZOKUWA NAZO KABLA YA KUFARIKI ILIBIDI MWILI WA MAREHEMU USAFIRISHWE
HADI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO
ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA
KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI
YA PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA.
§ TARATIBU
ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI
YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA
NA KUJUA AINA YA DAWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.
§ KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA
KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA KWANI SIO TU NI KINYUME CHA
SHERIA ZA NCHI BALI PIA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA
RAI KWA WAKAZI WA MBEYA NA TANZANIA
KWA JUMLA KUFIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MWILI WA
MAREHEMU.
[DIWANI ATHUMANI-
ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Picha kwa Hisani ya Mbeya Yetu.
0 comments:
Post a Comment