Sunday, October 13, 2013

MASOGANGE NA UTATA WA SHERIA ZA MADAWA YA KULEVYA BONGO

Yule mwanadada msanii wa Kibongo Agnes Gerald maarufu kama Masogange iliyekuwa na kesi ya madawa ya kulevya Nchini Afrika Kusini inadaiwa ameshatua hapa Bongo wiki iliyopita. Mwanadada huyu ameachiwa baada ya kulipa faini ya Randi 30,000 (Tshs milioni 4.8) katika kesi iliyokuwa inamkabili.
Baada ya mwanadada huyo kuingia hapa  nchi vyombo au taasisi zinazohusika na kupambana na madawa ya kulevya vinasema havina shida ya kumchukulia hatua yoyote kwa kuwa alishahukumiwa Afrika Kusini.
Ikumbukwe kwamba mwanadada huyu alitoka na mzigo huo wa zinazosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya hapa nchini Tanzania na kupita katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kabla ya kwenda kukamatwa nchini Afrika ya Kusini.
Kimtazamo sisi tulikuwa tunaona hii Taasisi ya kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya ingekuwa ya kwanza kumshikilia hapa nchini ili aweze kuwasaidia kujua au kutaja mzigo ule ulikuwa wa nani au ametumwa na nani?.Sasa wanaposema kisheria kama ameshapewa hukumu nje ya nchi akiwa hapa sheria hazina habari naye naona kuna haja ya kutunga sheria zenye kubana zaidi biashara hii haramu inayoangamiza vijana hapa nchini ambao ndio nguvu kazi ya Taifa letu.

0 comments:

Post a Comment