Wiki hii imekuwa ya majonzi makubwa kwa Watanzania baada ya miili ya mashujaa wetu wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania wapatao saba kuwasili nchini na kuagwa kwa heshima zote hapa jijini Dar kabla ya kupelekwa kuzikwa nyumbani kwao.Wanajeshi hawa walipatwa na mauti haya huko Darfur nchini Sudani baada ya kuvamiwa na waasi wakiwa katika majukumu ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.Hapa msafara wa magari ukipita maeneo ya Bamaga ukitokea Lugalo Jeshini kuelekea Upanga tayari kwa shughuli za kuwaaga mashujaa hao.
0 comments:
Post a Comment