Sunday, February 3, 2013

WAVUVI WADOGO WADOGO KATIKA MWALO WA KAWE BEACH JIRANI NA PICOLLO HOTELI,

Kuona Vizuri picha hii bonyeza mara mbili juu ya picha hii.
    
    Wahenga hunena kwenye miti mingi hakuna wajenzi, hili linajidhihilisha kwa nchi yetu ambayo ina maliasili za kutosha kwa upande wa bahari ya Hindi,samaki na mazao mengine ya bahari ambayo mpaka sasa uvunaji wake ni duni na wa kitoto kabisa maana nyenzo tunazotumia kwa wavuvi wetu bado ni zile zile walizotumia wazee wetu kabla hata wakoloni hawajaingia Afrika.
   Hapa baadhi ya wavuvi katika pwani ya Kawe wakirudi jioni baada ya kutoka asubuhi kwenda kutega samaki.Kwa kweli cha kusikitisha ni kwamba kiasi cha samaki wanachorudi nacho ni kidogo sana kulingana na mda waliotumia kukaa baharini mchana kutwa.
    Tunaomba Serikali iangalie sekta hii ya uvuvi mdogo ili uwe uvuvi wa tija kwa wavuvi hawa katika kujipatia vipato vikubwa kukidhi mahitaji yao ya kila siku. 

0 comments:

Post a Comment