Zitto Kambwe akitoka Mahakama
Kuu jana na
Mwanasheria wake Albert Msando.
Hali imekuwa tete kwa Mbunge wa Kigoma
Kaskazini Zitto Kabwe ambaye hivi karibuni ameingia katika mgogoro mzito na
chama chake cha CHADEMA,na kuvuliwa uongozi na nyadhifa zote ndani ya chama
hicho.
Zitto aliandika barua ya
utetezi kwa Baraza kuu la chama hicho akiliomba limpe nafasi ya kujitetea
kufuatia kamati kuu ya chama hicho kumtuhumu kwa makosa 11 na kumvua nyadhifa
hizo lakini Baraza Kuu halikumjibu barua yake na hivyo Kamati Kuu ya chama
hicho leo ilikuwa na kikao cha kumjadili na inasemekana katika kikao cha leo
lengo kuu ni kumvua uanachama wa CHADEMA.
Kufuatia hali hiyo Zitto Kabwe
alienda kufungua kesi Mahakama Kuu kupitia mwanasheria wake Albert Msando
akiomba mahakama izuie Kamati Kuu ya CHADEMA kumjadili mpaka pale kesi yake ya
msingi ndani ya CHADEMA itakaposikilizwa.
Hivyo Mahakama Kuu ilikubali ombi la
Zitto Kabwe na kumpa ushindi dhidi ya mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lisu
ambaye mapingamizi yake yalitupiliwa mbali na Mahakama Kuu.
Kitendo cha Zitto
kukimbilia mahakamani kinaonesha kuwa hali ni mbaya kwa mwanasiasa huyo ndani
ya CHADEMA na hakuna hata mtu mmoja wa kumkingia kifua ndani ya chama hicho ili
kuweza kumnusuru na upepo mbaya uliompitia ndani ya chama hicho.Na sasa
amekalia kuti kavu na yupo mbioni kutimuliwa ndani ya chama hicho mda wowote
kuanzia sasa.
0 comments:
Post a Comment