Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh.Edward Lowasa kwa kipindi kirefu amekuwa katika harakati za kuchangia harambee mbalimbali hapa nchi makanisani na katika vikundi vya vijana kiasi kwamba wadau wa kisiasa wanasema ni katika harakati zake za kujaribu kuwa karibu na wananchi ili aweze kugombea urais kwa mwaka 2015.
Lakini hivi karibuni amewashitua wadau wengi wa siasa pale alipokuwa akifanya idaba ya shukrani ya kumaliza mwaka 2013 na kuuanza mwaka wa 2014 ibada iliyofanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Monduli,alitamka wazi kuwa sasa anaanza safari ya matumaini kwa Watanzania,safari ya kutimiza ndoto zake kwa Watanzania za kuwapa elimu bora bure,huduma ya maji safi na salama maisha bora Watanzania wote.
Kauli hii imetafsiriwa na wadau wa siasa kuwa inaonesha dhahiri kuwa Mh.Lowasa ana nia haswa ya kugombea urais hapo mwaka 2015.Ingawa hajatamka wazi lakini kwa harakati zake hizi kwa muda mrefu inaonesha anakitaka kiti hicho kwa udi na uvumba.Sisi tunasubiri tuone kama ni mbio za sakafuni au la.
0 comments:
Post a Comment