Mshambuliaji hatari wa Simba Ramadhani Singano akijaribu kumtoka mchezaji wa Kagera Sugar Malegesi Mwanga.
Timu ya Simba FC imelazimishwa kwenda sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar ya Kagera katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara mchezo uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.Simba walikuwa wa kwanza kupata bao lao katika kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wao Asimi Tambwe.Kagera Sugar waliingia kwa kasi katika kipindi cha pili na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Simba na katika dakika za mwisho za mchezo wakapata penati baada ya Joseph Owino kumtendea madhambi Daudi Jumanne wa Kagera Sugar katika eneo la hatari. Penati hiyo ilipigwa na Salum Kanoni na kusawazisha bao hilo kitendo ambacho kiliwachukiza washabiki wa Simba na kuanza vurugu huku waking'oa viti vya Uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment