Mtoto huyu akitembea juu ya reli akitokea Mabibo kuelekea Tabata jirani na "Yard" za AMI Tabata relini maeneo ya Gazeti la Mwananchi.Kitendo hiki ni hatari kwa kuwa reli hii kwa sasa inatumika kwa ajili ya kusafirisha abiria Dar es Salaam.Hivyo tahadhari inatakiwa kwa wazazi kuwakumbusha watoto wao kuacha kucheza pembezoni mwa reli hii au kupita katikati ya reli hii kwa kuwa inaweza kusababisha ajali wakati wowote. Tayari wiki iliyopita majira ya asubuhi tumeshuhudia ajali eneo la Mabibo Muleba Toyota Land Cruizer lilipogonga Treni katika makutano ya barabara na reli.
0 comments:
Post a Comment