Saturday, December 15, 2012

MCHUUZI WA BIASHARA NDOGONDOGO MAENEO YA MOROCCO JIJINI DAR ES SALAAM.AINA HII YA BIASHARA IMEKUWA IKIPOTEZA MAPATO KWA SERIKALI.

Kijana mfanyabiashara ndongondogo maeneo ya Morocco Jijini Dar es Salaam akiwa amebeba vitu mbalimbali vya dukani kwa ajili ya kuviuza kwa watu waliokuwemo kwanye magari wakiwa kwenye foleni ya mataa.
Biashara hii inahusisha vitu vya madukani ambopo wakati kijana huyu anafanya mauzo hakuna risiti yoyote inayotolewa hivyo kusababisha  Serikali kupoteza mapato yake.Inasadikiwa bidhaa hizi ambazo nyongine ni za thamani kubwa hupewa na wafanyabiashara wa Kiasia ambao baada ya kuuza wanapewa kamisheni yao.
Pamoja na kwamba vijana wanapata ajira lakini mamlaka husika iangalie upya jinsi ya kuweza kupata mapato katika biashara hizi au ikibidi wanaweza kuzipiga marafuku au kuzitafutia sehenu maalum ili waweze kukusanay mapato yake.
 
Je,wewe mzalendo una maoni gani?

0 comments:

Post a Comment