Wednesday, January 1, 2014

PICHA ZA JAMAA ALIYETAKA KUJIRUSHA JUU YA MNARA MAENEO YA UBUNGO AKISHINIKIZA KUONANA NA RAIS KIKWETE ILI AMPE KERO ZAKE.

 Jamaa mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja jana mchana alipanda juu ya mnara wa simu maeneo ya Ubungo jirani na ofisi za Shirika la Viwango nchini TBS.Jamaa huyo alisema anataka Rais Kikwete aje ili ampe kero yake ya kufungwa miaka sita (6) jela kwa kubambikiwa kesi na Polisi.Hata hivyo askari wa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji walifanikiwa kumpandia juu na kumshawishi ashuke hivyo wakashuka naye salama kutoka juu ya mnara huo.
  Askari wa Uokoaji wakishuka na jamaa huyo.
Jamaa akiongea na waandishi wa habari.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakishuhudia tukio hilo.
Umati wa watu wakifuatilia kwa makini mkasa huo wa aina yake.

Picha kwa hisani ya Mpekuzi.

0 comments:

Post a Comment