Mbunge Zitto Kambwe wa Kigoma
Kaskazini aliyevuliwa nafasi zote za uongozi hivi karibuni katika chama chake
cha CHADEMA amefanya mikutano mitatu(3) mkoani Kigoma kuanzia Jumamosi
akianzia Mwandiga alipozaliwa na kukulia,akaenda Kasulu na Jumatatu alikuwa
Kigoma mjini katika eneo la Mwanga Uwanja wa Community Center ;huku akipata
mapokezi makubwa kushinda aliyopata Katibu Mkuu wake Dr.Wilbroad Slaa
alipofanya ziara mkoani humo.
Kufuatia hali hiyo Dr.Slaa
amempiga marafuku kufanya mikutano hiyo akidai mikutano yake siyo halali
anastahili kufanya mikutano yake Jimboni kwake tu Kigoma Kaskazini.
Hata hivyo Zitto Kabwe alimjibu
kwa kumpinga Dr.Slaa na kusema kwa mujibu wa Katiba yeye ni Mbunge na
anaruhusiwa kufanya mikutano sehemu yoyote ndani ya Tanzania labda kama
CHADEMA imemfukuza katika nafasi yake ya Ubunge basi waseme.
Amesema
ataendelea kufanya mikutano kama kawaida akitoka Kigoma ataenda
Mpanda,Tabora,Shinyanga,Mwanza na ataenda mpaka Arusha pia.
0 comments:
Post a Comment