Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana ametengua uteuzi
wa Mawaziri wanne Khamis Kagasheki(Maliasili na Utalii),David Mathayo (Mifugo
na Uvuvi),Emanuel Nchimbi(Mambo ya Ndani) na Shamsi Vuai Nahodha(Ulinzi na JKT)
kufuatia shutuma nzito dhidi yao katika sakata la Operesheni Tokomeza Ujangili.
Akifanunua Bungeni jana kuhusu sakata hilo Waziri
Mkuu Mizengo Pinda alisema Operasheni yenyewe ilikuwa na lengo zuri ila
utekelezaji wake ndio uliokuwa na dosari ambayo iliambatana na ukiukwaji mkubwa
wa haki za binadamu.
Bunge limeahirishwa leo mpaka tarehe 6 Mei,2014
0 comments:
Post a Comment