Mwanadada
matata wa Bongo Movie Aunt Ezekiel ambaye alibadili dini kutoka Ukristo na
kuingia Uislam akiitwa jina la Rahma na kuolewa kwa ndoa ya kiislam na Bwana
Sunday Demonte ametabainisha kuwa anatamani kuokoka na kurudi kwenye dini yake
ya zamani ya kikristo. Staa huyo aliyanena hayo alipohojiwa na GPL nyumbani
kwake Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Alisema
mara nyingi akisikia mafundisho na mahubiri ya kikristo anajisikia faraja sana
na anapenda kusikiliza nyimbo za injili.
Baadhi
ya wapenzi wake wanadai kuwa binti huyo atakuwa ameshindwa kuishi kwa maadili
ya kiislam ndio maana anataka kurudi kwenye ukristo na wengine walifika mbali
na kudai alikuwa anaudanganya umma wala hakuwa na nia ya kuingia uislam ndio
maana sasa anataka kuukimbia uislam.
0 comments:
Post a Comment