Wabunge vijana na machachari wote wa CHADEMA
Zitto Kabwe na Godbless Lema wameingia katika vita kali ya maneno kupitia
mitandao ya jamii kuhusu masuala ya posho kwa vikao vya bunge.
Godbless Lema amekuwa kimtuhumu Zitto kuwa ni
mnafiki mkubwa katika suala la posho ambazo anazikataa kwa vikao vya bunge
ambazo kila kikao ni Tshs 70,000/= huku akipokea posho za vikao vya Mashirika
ya Jamii kama mwenyekiti wa PAC ambazo ni kati ya Tshs (500,000/= -
1,000,000/=) kwa kikao kimoja.Lema alijinasibu kupitia walaka alioutoa kwa
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa kama Zitto ni mzalendo
angekataa na posho hizo pia ili zikasaidie wajawazito,maji vijini,shule za kata
na maendeleo mengine mengi.Aliendelea kumshambulia Zitto kuwa ni mnafiki na mtu
anayetaka sifa tu kwa wanachi wakati sifa hizo za uzalendo hana.
Zitto kabwe
akijibu tuhuma hizo kwa kuandika katika ukurasa wake wa
"facebook" amesema yeye binafsi alishafunga mjadala wa posho toka
8/6/2011 alipoacha kuchukua posho ili isaidie katika maendeleo ya jamii kama
mama wajawazito,shule za kata na maendeleo mengine mengi.Kama kuna mtu
anachukia kwa uamuzi wake huo na achukie tu lakini yeye binafsi hatapokea
posho hiyo ya vikao vya bunge.
Wabunge hawa ambao
wanamvuto mkubwa wa kisiasa hapa nchini wameamua kupigana vita hivyo vya maneno
kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari bila kupitia vikao vya chama
chao CHADEMA.Hali hiyo ya sinto fahamu imewashangaza wananchi wengi ambao
bado wanatafakari mwisho wa vita hii katika mitandao ya kijamii itaishia wapi.
0 comments:
Post a Comment