Rais Jakaya Mrisho kikwete na viongozi wa vyama vya upinzani katika picha ya pamoja Ikulu Dar es Salaam.Rais Kikwete alikutana na wapinzani kujadili hoja ya kusainiwa kwa mswada wa sheria wa Katiba Mpya ambao wapinzani hao waliususia Bungeni kwa kuwa ulikuwa na mapungufu.Hivyo walikuwa wakiomba Rais asiusaini kwanza kwa kuwa bado ulikuwa na mapungufu.Hata hivyo Rais alikuwa amekwisha saini mswada huo na kuwaomba wapinzani walete hayo mapendekezo yao kwa Serikali ili yaweze kuingizwa katika mswada huo.
0 comments:
Post a Comment