Wednesday, October 30, 2013

EDWARD SNOWDEN JASUSI ALIYEISALITI MAREKANI SASA AITESA NCHI HIYO.

    Edward Snowden jasusi wa kimarekani aliyeasi na kuomba hifadhi nchini Urusi amekuwa mwiba kwa Shirika la Kijasusi la Marekani kwa kuwa anatoa siri mbalimbali za Shirika hilo kwa sasa. Marekani wamefanya kila jitihada za kutaka arudishwe nchini humo imeshindikana.
   Hivi sasa ametoa taarifa kuwa Marekani inafuatilia mawasiliano ya nchi mbalimbali duniani na viongozi wa nchi hizo jambo ambalo limezua mtafaruku kwa viongozi duniani na kusababisha Umoja wa Ulaya kutuma wajumbe wake Marekani ili kupata ukweli wa jambo hilo.
   Katika taarifa ya hivi karibuni Snowden amesema Marekani huangalia simu zipatazo milioni 60 kwa mwezi kwa nchi ya Hispania.

0 comments:

Post a Comment