Hii ndio hali ya mapipa mengi ya taka hapa Jiji Dar es Salaam yanavyoonekana. Pipa hili lipo maeneo ya mataa ya makutano kati ya barabara ya kwenda Kinondoni Makaburini na Ali Hassani Mwinyi jirani na Banki ya Stanbic. Kwanza tunashukuru Halmashauri za jiji hili kwa hatua ya kwanza kuweka mapipa haya na wananchi kuitikia wito wa kuweka taka katika mapipa haya.
Changamoto imayojitokeza sasa ni jinsi ya kuyahudumia mapipa haya,inaonekana halmashauri za Jiji zinashindwa kuzoa taka hizo katika mapipa haya hali inayosababisha yajae na hata kumwagika kiasi kwamba hata hayavutii tena kwa mtu kwenda kutupa taka hapo.
Pichani ni pipa likiwa limejaa kufungwa kamba ili taka zisiendelee kumwagika.Tunaomba Halmashauri za Jiji kijipanga upya katika kuzitoa taka hizi kwenya haya mapipa za taka.
0 comments:
Post a Comment