Kusoma na kuona vizuri picha hii ponyeza "Read more" |
Leo ni siku ya Wanawake Duniani,pichani wanaonekana Wanawake wawili wakiwa wanapita barabarani maeneo ya Baraza la Mitihani jijini Dar es Salaam huku wakiwa wamebeba mihogo mibichi na matango wakipita kutafuta wateja.Hii ndio hali halisi ya Mwanamke wa Kitanzania na Wakiafrika katika kujitafutia pesa ya kujikimu kimaisha kila siku iendayo kwa Mungu maana kwa biashara hii hawezi kupata fedha za kuweka akiba ni lazima kila siku aende sokoni kununua mihogo na matango ili auze siku hiyo na inamchua muda mrefu kuzunguka mitaa ya Jiji la Dar es Salaam akitafuta wateja.Lakini kwa nchi zilizoendelea huwezi kumkuta Mwanamke akifanya bishara hii hivyo tuna kila sababu kama nchi katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani kujadili ni jinsi gani tunaweza kumkwamua Mwanamke katika maisha haya magumu yanayomkabili kila kukicha.
0 comments:
Post a Comment