Tuesday, February 26, 2013

HALI YA USAFIRI KWA WANAFUNZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM BADO SI NZURI WANAFUNZI WAMEKUWA WAKIPATA USUMBUFU MKUBWA SANA WAKATI WA ASUBUHI NA JIONI KATIKA KUPATA USAFIRI

 
Wanafunzi wakihangaika kutafuta usafiri katika kituo cha basi cha Mabibo ili waende shuleni majira ya asubuhi.Hali hii imekuwa na usumbufu mkubwa kwao kwa muda mrefu na bado hakuna jitihada za makusudi na endelevu za kuwasaidia watoto hawa ili wakasafiri katika utaratibu mzuri.
Hapo awali kulikuwa na mradi wa mabasi ya wanafunzi ukafa na kuna wadau walitoa  mabasi kwa kampuni ya Usafirishaji Dar (UDA) mfano bank ya CRDB lakini mabasi hayo hayakudumu mda mrefu yanakufa.
Hapa kama nchi tunahitaji utatuzi wa kivitendo kwa Serikali kuwasaidia wanafunzi hawa kuwa na usafiri wa uhakika ili wasipoteze muda mwingi katika kusafiri wakati wa kwenda na kurudi shuleni.
Waziri wa Uchukuzi pamoja na mambo mazuri na mazito unayofanya ili nalo uliwekee mkakati maalumu wa kulitatua.

0 comments:

Post a Comment